Mohammad Hassan Ali Al-Kabari aliyasema hayo katika mahojiano na IQNA kuhusu shakhsia ya Qur’ani ya Kiongozi huyo shahidi.
Akirejelea kiwango cha mapenzi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika kuhifadhi, kusoma, na kutafakari aya za Qur’ani Tukufu, alisema: “Shahidi Imam Khamenei kwa kweli aliishi kwa ajili ya kufikia daraja ya ushahidi, na katika maisha yake yote, alihuisha mapenzi ya kina kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani ya nyoyo za watu. Mwenyezi Mungu alimjalia baraka ya ushahidi kutokana na unyofu wake kwa Qur’ani. Kwa njia hii, Mwenyezi Mungu alifanya nyoyo za watu ziwe na shauku ya kumtii na kumpenda.”
Alisema kuwa utii wa Kiongozi Shahidi kwa Qur’ani Tukufu ulimfanya Mwenyezi Mungu ainue hadhi na mamlaka yake na kumpa heshima na nguvu, akiongeza kuwa yeyote anayekiheshimu Kitabu cha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atainua hadhi na hatima yake.
“Kiongozi Shahidi alionyesha ahadi yake thabiti kwa usomaji wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na taasisi za kuhifadhi Qur’ani kote nchini Iran na katika maeneo mengi ya medani ya Jihad. Kwa hakika, kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kulikuwa ndiyo mantiki na msingi wa kila jambo; uhusiano na Neno la Mwenyezi Mungu, kufahamiana na Qur’ani, kusikiliza aya, na kukiheshimu Kitabu cha Mwenyezi Mungu vimeingiliana na ngozi na damu ya kila mujahid.”
Al-Kabari alilinganisha uadui wa makafiri dhidi ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na ukosefu wa uungaji mkono wa wanafiki kwa Kitabu hicho, na mwenendo wa kivitendo na mkakati wa hekima wa Kiongozi Shahidi.
“Tuliona umakini wa Kiongozi Shahidi kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu kama jibu la kitabia dhidi ya kiburi cha makafiri. Kile alichokifanya Kiongozi Shahidi ni njia ya wale wanyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, wanaolea vizazi kupitia vitendo, tabia, na njia iliyonyooka.”
Msomaji huyo wa Qur’ani kutoka Yemen aliongeza: “Yeyote anayesoma mafunzo ya Kiongozi Shahidi, ambaye aliishi katika ulinzi wa Qur’ani, na yeyote anayesoma maandiko yake na yale yaliyosambazwa kupitia vyombo vya habari, pamoja na tafsiri zake za aya tukufu, iwe katika ujana wake au wakati wa uongozi wake, atatambua kuwa Kiongozi wetu Shahidi alijua kuwa furaha ya kutafakari Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndiyo pepo ya dunia hii na chanzo cha upanuzi wa vifua vya waumini.”
Alimalizia kwa kurejelea ushikamanifu wa Kiongozi Shahidi kwa maisha matukufu ya Mtume Muhammad (SAW) na kusema kuwa yote hayo huongoza kwenye ukomavu, na kiongozi huyo wa hekima aliilea Ummah wa Kiislamu katika njia ya ukomavu.
3498314