IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kutekeleza mafunzo ya Ahul Bayt wa Mtume SAW ni kupambana na ukafiri, unafiki

22:47 - February 24, 2017
Habari ID: 3470867
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kuwafuata sawasawa Maimamu maasumu AS ni kuwafuata kivitendo watukufu hao na kudumisha mapambano dhidi ya ukafiri na unafiki.
Ayatullah Sayyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
ameyasema hayo Alhamisi mjini Tehran alipohutubia mkutano wa kundi la malenga na washairi wa kidini  zikiwa zimebakia siku chache kabla ya shughuli ya kukumbuka tukio chungu la kufa shahidi binti wa Mtume wetu Muhammad SAW, Bi Fatimatu Zahra SA.
Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, kuwa, kuungana kwa matukio ya zama za awali za Uislamu na matukio ya kipindi cha sasa ni ujumbe muhimu kwa malenga na washairi wa kidini na kuongeza kuwa: Mtume Muhammad (saw) na Maimamu watoharifu katika kizazi chake walikuwa wakipambana vikali na dhulma, madhalimu, ukafiri, unafiki na ufuska na kwa sababu hiyo waliuawa shahidi na watawala madhalimu na waovu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, kuwafuata sawasawa Maimamu maasumu ni kuwafuata kivitendo watukufu hao na kudumisha mapambano dhidi ya ukafiri na unafiki. Ameongeza kuwa: Mapambano dhidi ya ukafiri na unafiki wa kimataifa ni rahisi na jambo linalowezekana katika Jamhuri ya Kiislamu lakini tangazo lolote la kujibari na kujitenga na Marekani chini ya kivuli kiovu cha baadhi ya tawala za eneo la Mashariki ya Kati hufuatiwa na hasira na jibu kali la tawala hizo.

Ayatullah Khamenei amesema, mapambano dhidi ya madhalimu hayahusu tu mapambano ya kutumia silaha na upanga na kwamba hii leo suala la kulingania dini duniani linachukua nafasi ya kwanza na inawezekana kupambana na madhalimu kwa kutumia maneno na mashairi. Amesisitiza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mifano mizuri sana na ya kutia matumaini katika uwanja huo.

Suala la mtindo wa maisha na wajibu wa malenga na washairi wa kidini mkabala wake, ni miongoni mwa masuala yaliyoashiriwa na Kiongozi Muadhamu katika mkutano huo. Amesema kuwa: Hii leo barani Ulaya na Marekani kumeanzishwa vituo na taasisi zenye malengo maalumu kwa ajili ya kubadili mtindo wa maisha katika nchi zisizo za Kimagharibi hususan Iran ya Kiislamu.

Ayatullah Khamenei amesema lengo la hujuma inayofanywa dhidi ya mtindo wa maisha wa Kiislamu ni kuanzisha irada, azma na harakati inayoowana na matakwa ya taasisi za Kimagharibi. Ameongeza kuwa, mkabala wa hujuma hiyo, haitoshi kujihami na kujiwekea uzio, bali tunaweza kutekeleza majikumu yetu kwa kubainisha na kuweka wazi mtindo wa maisha wa Kiislamu na kueleza mafundisho na misingi ya kimaadili, kisiasa na kiutamaduni katika kalibu na sura ya mashairi.

3576583



captcha