Mkutano huo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iraq, Abdul Amir Al-Shammari, na ulihudhuriwa na maafisa kadhaa waandamizi wa polisi na usalama.
Waziri wa mambo ya ndani alielezwa kuhusu hatua zilizochukuliwa na taasisi za usalama na kutoa maagizo ya kuboresha maandalizi.
Alisisitiza umuhimu wa uratibu na ushirikiano kati ya wizara na mashirika husika ili kuhakikisha usalama wa waumini watakaozuru Haram ya Imam Jawad (AS) katika eneo la Kadhimayn.
Tarehe 30 ya mwezi wa Hijri wa Dhu al-Qi’dah, ambayo mwaka huu inaangukia Mei 27, inaadhimisha kumbukumbu ya kufa shahidi Imam Jawad (AS).
Kwa mnasaba huu, wafanyaziara na wafuasi wa Ahl-ul-Bayt (AS) husafiri hadi maeneo matakatifu nchini Iraq, ikiwemo mji mtakatifu wa Kadhimiya, kwa ajili ya maombolezo.