IQNA

Ziyara ya Kidini

Msikiti wa Mtume (SAW) umekaribisha wageni zaidi ya milioni tano kwa wiki moja

21:23 - September 06, 2024
Habari ID: 3479390
IQNA - Mamlaka Kuu ya Utunzaji wa Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume huko Saudi Arabia iliripoti kwamba Msikiti wa Mtume maarufu kama al-Masjid an-Nabawi  uliwapokea Waislamu zaidi ya milioni tano wiki iliyopita.

Huduma zilizotolewa zililenga kuhakikisha uzoefu mzuru wa ibada na Swala, kulingana na Shirika la Habari la Saudi.

Takwimu za mamlaka hiyo zilionyesha kuwa Waislamu 483,822 walitembelea al-Masjid an-Nabawi huku wageni 250,725 wakiswali katika Al Rawda Al Sharifa, ambapo kaburi la Mtume Muhammad (SAW) liko.

Shughuli hizi zilisimamiwa kwa ustadhi ili kuhakikisha hakuna msongamano  ambapo pia kulipangwa nyakati maalumu za Swala na ibada  kwa wanaume na wanawake. Zaidi ya hayo, watu 74,486 walitumia huduma za utafsiri.

Zaidi ya hayo, tani 1,640 za maji ya Zamzam zilisambazwa miongoni mwa waliofika katika eneo hilo takatifu.

Mamlaka pia ilitoa milo ya futari 143,142 kwa watu waliofunga katika maeneo maalum ndani ya al-Masjid an-Nabawi .

3489779/

captcha