IQNA

Mashindano ya Qur'ani Hamburg yalenga kutafuta vipawa

16:57 - March 13, 2017
Habari ID: 3470892
IQNA-Kati ya malengo ya mashindano ya Qur'ani ya Waislamu barani Ulaya ni kutafuta na kubaini vipawa vilivyopo vya Qur'ani barani humo.

Hayo yamedokezwa na Hujjatul Islam Ismaili Ansari, mkuu wa Darul Qur'an katika Kituo cha Kiislamu cha Hamburg, Ujerumani. Ameongeza kuwa lengo jingine la mashindano hayo lilikuwa ni kuimarisha kiwango cha ujuzi na ufahamu wa Qur'ani Tukufu miogoni mwa vijana.

Duru ya tano ya Mashindano ya Qur'ani ya Bara Ulaya yalifanyika Hamburg kuanzia Machi 10-12.

Wanaharakti 160 wa Qur'ani walishiriki katika mashindano hayo kutoka nchi mbali mbali za Ulaya.

Hujjatul Islam Ansari ambaye pia ni msimamizi wa masuala ya kijamii na kiutamaduni katika Kituo cha Kiislamu cha Hamurg amesema kiwango cha mashindano ya mwaka huu kilikuwa cha juu ikilinganishwa na miaka ya nyumba. Aidha amesema idadi kubwa ya washiriki walikuwa katika vintego vya kuhifadhi na ufahamu wa Qur'ani.

3583457

captcha