IQNA

Mashindano ya 4 ya Qur’ani Tukufu ya Ulaya Kaskazini

9:21 - August 12, 2016
Habari ID: 3470517
Mashindano ya 4 ya Qur’ani Tukufu Ulaya Kaskazini yameanza Ijumaa hii katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo yanafanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Imam Ali AS ambapo kuna washiriki 92 kutoka Sweden, Norway, Denmark na Finland.

Mashindano hayo yatakuwa na kategoria kadhaa zikiwemo qiraa ya Qur’ani, tarteel, hifadhi, Adhana na ufahamu wa Qur’ani Tukufu.

Jopo la majaji katika mashindano hayo lintakuwa na wataalamu kutoka Denmark, Ujerumani, Iran na Uholanzi.

Majaji hao ni pamoja na Seyed Mohammad Javad Mousavi Dorchei kutoka Iran, Seyed Yahya Hosseini kutoka Denmark na Hassan Sadeqi Shouredeli kutoka Ujerumani.

Waandalizi wa mashindano hayo wanasema wanalenga kustawisha utamaduni na mafundisho ya Qur’ani, kubaini vipawa vya Qur’ani na kuimarisha umoja baina ya jamii ya Waislamu Ulaya Kaskazini.

Halikadhalika mashindano hayo yanatazamiwa kuwa jukwaa la wasomaji na wanaohifadhi Qur’ani kukutana na kubadilishana mawazo.

Aidha washindi katika mashindano hayo watawakilisha nchi zao katika mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani Tukufu nchini Iran mwakani.

3521990

Kishikizo: qurani iqna ulaya sweden
captcha