IQNA

Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani kwa lugha ya Kihispania katika maonyesho ya vitabu Tehran

19:10 - May 13, 2017
Habari ID: 3470977
TEHRAN (IQNA)-Tafsiri ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kihispania ni kati ya vitabu katika Maonyesho ya Kimatiafa ya Vitabu ya Tehran yanayomalizika leo.

Tafsiri hiyo ya Qu'rani kwa lugha ya Kihispania imeonyeshwa katika kibanda cha Shirika la Uchapishaji la Sozler katika Maonyesho ya Kimatiafa ya Vitabu Tehran. 'Tafsir Maanawi' imetajwa kuwa tafsiri ya kwanza ya Qur'ani kwa lugha ya Kihispania. Kwa mujibu wa Bw. Rahman Mirhassani, Shirika la Uchapishaji la Sozler hadi sasa limechapisha 'Tafsir Maanawi' kwa lugha 60 duniani.

Kati ya vitabu vingine vinavyohusiana na Qur'ani katika kitengo cha nchi za kigeni katika Maonyesho ya Kimatiafa vya Vitabu Tehran ni kitabu chenye anuani ya, "Maryam katika Qur'ani", "Masomo ya Qur'ani Leo" ambayo kimeandika na Angelika Neuwirth na kichapisha na shirika la Routledge la Uingereza. Halikadhlika kuna tarjama za Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kiingereza za Yusuf Ali na Muhmmad Assad.

Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu Tehran yalianza Mei 3-13 na wasimamizi wa maonyesho wanasema vitabu vyenye thamani ya dola milioni 10 vimeuzwa katika maonyesho ya mwaka huu.

3462805
captcha