Hii ni katika hali ambayo Trump anajulikana kuwa kinara wa chuki dhidi ya Uislamu duniani huku Saudia nayo ikiwa ni mlezi mkuu wa kiroho wa magaidi wakufurishaji duniani ambao wanafuata itikadi ya Kiwahhabi ambayo ni itikadi rasmi Saudi Arabia.
Trump alipata umashuhuri katika kampenzi zake kwa kueneza fikra na mitazamo ya chuki dhidi ya Uislamu na pia baada ya kuchaguliwa alipitisha sheria ya kuwapiga marufuku watu kutoka nchi kadhaa za Kiislamu kuingia nchini humo. Saudia nayo ni kitovu cha fikra za Kiwahhabi ambazo zinatumiwa na magaidi wa makundi kama vile ISIS, Al Qaeda, Taliban, Boko Haram na Al Shabab.
Mnamo Mei 20, Trump akiwa ameandamana na mke wake waliingia Riyadha kwa ajili ya kikao kilichotajwa kuwa ni cha Uislamu na Marekani mjini Riyadh.
Viongozi wa Saudi Arabia na Marekani wamesaini makubaliano kadhaa katika nyanja mbalimbali yakiwemo masuala ya kijeshi, yenye thamani ya dola bilioni 380. Aidha mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud amemvisha Trump mkufu wa dhahabu wenye gharama kubwa na kucheza naye mziki wa dansi ya kijahilia.
Makubaliano hayo yaliyofikiwa Jumamosi, yalitiwa saini mjini
Riyadh baina ya Rais Donald Trump wa Marekani na Mfalme wa Saudia, Salman bin
Abdulaziz Al Saud. Kufuatia utiaji saini huo, White House imedai kuwa,
makubaliano hayo muhimu ya kijeshi baina ya Saudia na Marekani yana lengo la
kuiruhusu Washington kutoa ulinzi kwa nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi kutokana
na hatari ya ugaidi.
Hayo yanajiri katika hali ambayo sehemu kubwa ya silaha zinazonunuliwa na Saudia kutoka Marekani, ndizo zinatumika kuishambulia nchi jirani ya Kiislamu ya Yemen huku sehemu nyingine ya silaha hizo ikigawiwa na Riyadh kwa makundi ya kigaidi yanayotekeleza jinai kubwa nchini Iraq, Yemen na Syria. Safari ya Rais Trump nchini Saudia na ambayo ni ya mara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa Marekani nje ya nchi tangu alipochaguliwa kuwa rais, imekosolewa sana na Waislamu duniani hasa kutokana na rais huyo kuwa na chuki kali dhidi ya Uislamu na wafuasi wa dini hii tukufu ya mbinguni.
Katika tathmini jumla kuhusu malengo hasa ya safari ya Trump
katika Asia Magharibi au Mashariki ya
Kati, tunaweza kusema kuwa katika miaka ya hivi karibuni Marekani imekuwa
ikifuatilia malengo yaliyo na utata mkubwa katika eneo na madamu nchi hiyo
itaendelea kufuatilia malengo hayo haramu ni wazi kuwa itaendelea kuitazama
Iran, ambayo imesimama imara mbele ya malengo hayo, kuwa ni tishio. Kwa msingi
huo tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na rais huyo wa Marekani kuwa Iran
inaunga mkono ugaidi si jambo geni. Suala lisilo na shaka ni kuwa Trump
ameonyesha kuwa na tamaa na pupa kubwa katika kuingilia masuala ya Mashariki ya
Kati lakini kwa kutilia maanani ukosoaji na upinzani mkubwa ambao umekuwa
ukimkabili katika ngazi za kimataifa kuhusu misimamo yake isiyo ya kimantiki,
bila shaka rais huyo hataweza kubuni muungano imara wa uhasama dhidi ya Iran
wala kutoa uungaji mkono wa kutosha kwa watawala wa Saudi Arabia kama
wanavyotarajia.
3601610