Waislamu wa Sweden wameongeza sauti yao kulaani kitendo cha Mfalme Salman kumpa mkono Melania Trump alipowasili mjini Riyadh akiwa ameandamana na mume wake.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu wa Sweden kupitia mtandao wa kijamii wa Insagram wamebainisha kuvunjwa moyo na kitendo cha mtawala wa Saudia kukiuka maadili ya Kiislamu
Kauli kali zaidi zimetolewa katika akaunti ya Instagram yenye jina la Islamisket ambapo waliochangia wameashiria mafundisho ya Kiislamu ambayo yanaharamisha mwanamke Mwislamu kumpa mkono mwanaume ajinabi kama ambavyo mwanaume Mwislamu haruhusiwi kumpa mkono mwanamke ajinabi.
Maoni hayo yameungwa mkono na idadi kubwa
ya watu katika ukurasa huo. Aidha nukta nyingine ambayo imewakasirisha Waislamu
ni kuwa, mke wa Trump na wanawake wengine waliokuwa katika ujumbe wa mtawala
huyo wa Marekani hawakuvaa hijabu wakati wakiwa ndani ya ardhi ya Saudi Arabia
katika hali ambayo siku chache baadaye walipomtembelea Papa Francis katika
makao ya Kanisa Katoliki Duniani huko Vatican walionekana wakiwa wamevalia
vitambaa kichwani kama ishara ya kumheshimu kiongozi huyo wa Wakristo. Wakuu wa
ofisi ya Trump wanasema ni sharti ya kiprotokali kwa wanawake kuvaa nguo ndefu
nyeusi na kitambaa cheusi kichwani wakati wa kutembelea Vatican. Hatahivyo
ofisi ya Trump imesema hawakutakiwa na wenyeji wao kuzingatia maadili ya mavazi
ya Kiislamu walipotembelea Saudia..
Mtawala wa Saudia anakosolewa na Waislamu kwa kukiuka mafundisho ya Kiislamu kwa sababu yeye na watawala wengine wote wa ukoo wa Aal Saudi hujinadi na kudai kuwa wao ni wahudumu wa Haram Mbili Takatifu za Kiislamu za Makka na Madina zilizo katika ardhi ya Hijaz ambayo imepachikwa jina la ukoo huo na kuitwa Saudi Arabia.
Mfalme huyu wa saudia anaupeleka wapi uislam?? Riyadh ndo nembo bado inachafuliwa na maadui wa kiislam ...
Urafiki gani huu wa mfadhili wa mauaji ya waislma na kitovu cha uislam duniani? Ama hakika adhabu atakayoitoa Allah katika hili itaangamiza wengi.. Mauziano ya silaha na mengine mengi yamemfanya Saudia kuwa kipofu kabisa