IQNA

Maonyesho ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yafunguliwa Tehran

11:07 - May 29, 2017
Habari ID: 3470999
TEHRAN (IQNA)-Maonyesho ya 25 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yameanza leo Alasiri katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini SA mjini Tehran.

Taarifa zinasema maonyesho hayo ya kimataifa yanahudhuriwa na taasisi 50 na pia kuna mashirika zaidi ya 297 ya uchapishaji. Kati ya mashirika hayo, 281 ni kutoka Iran na 16 ni ya kimataifa kutoka nchi kama vile Uturuki, Iraq, Lebanon na Syria.

Mkurugenzi wa maonyesho hayoa Abbas Nazarirad amemwambia mwandishi wa IQNA kuwa, maoneysho hayo yataendelea kwa muda wa siku 18. 

Aidha amesema kuwa milango ya maonyesho hayo itakuwa wazi kila siku kuanzia saa 12 jioni hadi saa sita usiku.

Afisa huyo amedokeza kuwa, nanra ya maonyesho ya mwaka huu ni "Qur'ani, Maadili na Maisha" na kwamba kutakuwa na hafla kadhaa kuhusiana na mada hii. Aidha mwaka huu kutakuwa na maonyesho maalumu yenye anuani ya: "Robo Karne ya Harakati za Qur'ani" ambapo washiriki watabainishiwa mafanikio ya maonyesho hayo ya kimataifa ya Qur'ani katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.

3462967


Jina:
Baruapepe:
* maoni:
captcha