IQNA

Magaidi wa ISIS waua Waislamu 30 katika hujuma msikitini Afghanistan

11:55 - August 26, 2017
Habari ID: 3471142
TEHRAN (IQNA) Magaidi wameuhujumu msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia mjini Kabul, Afghanistan na kuuawa waumini 30 waliokuwa katika Sala ya Ijumaa.

Taarifa zinasema magaidi hap walilipua bomu na kisha kumimina risasi wakati waumini walipokuwa wamekusanyika kwa ajili ya sala ya Ijumaa katika Msikiti wa Imam Zaman mjini Kabul na kuua shahidi watu wasiopungua 30 na kujeruhi wengine wengi.

Kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS au Daesh limetangaza kuhusika na jinai hiyo ambayo walioshuhudia wanasema ilitekelezwa na watu wanne. Maafisa wa usalama walifika katiak eneo la tukio na kukabiliana na magaidi hao waliokuwa wamewashikilia mateka waumini.

Mwezi uliopita pia magaidi wa ISIS waliuhujumu ubalozi wa Iraq mjini Kabul na baada ya hapo wakatoa onyo kwa Waislamu wote wa madhehebu ya Shia Afghanistan kuwa maeneo yao ya ibada yatahujumiwa. Punde baada ya onyo hilo, magaidi wa ISIS walishambulia msikiti wa Mashia katika mkowa Herat na kuua shahidi watu 32.

Wakati huo huo Iran imelaani vikali hujuma ya kigaidi dhidi ya msikiti wa Waislamu wa madhehebu ya Shia katika mji mkuu wa Afghanistan Ijumaa ambapo watu 20 waliuawa.


Katika taarifa, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Bahram Qassemi ametuma salamu za rambi rambi kwa serikali, taifa na familia za waathirika kufuatia jinai hiyo.

Ameongeza kuwa magaidi waliotekeelza hujuma hiyo wanalengo kuibua mivutano ya kimedhehebu na kuvuruga umoja wa taifa la Afghanistan lakini pamoja na hayo magaidi wanazidi kudhoofika siku hadi siku.

Qassemi ametoa wito kwa serikali na watu wa Afghanistan wavunje njama za maadui na waungaji mkono wao kupitia kudumisha umoja na kuimarisha usalama.

3634261

captcha