Kwa kuzingatia ukweli kuwa Uislamu ni dini ya amani, uadilifu, mantiki mbali na ni mfumo kamili wa maisha yenye kumeletea mwanadamu ufanisi wa dunia na akhera, iwapo dini hii tukufu itatangazwa kwa njia sahihi, idadi kubwa ya watu wasiokuwa Waislamu watanedelea kuvutiwa na Uislamu.
Uchunguzi uliofanywa pia umebaini kuwa, pamoja na kuwepo chuki dhidi ya Uislamu ambayo imetokana kwa kiasi kikubwa na ugaidi wa kundi la magaidi wa Kiwahhabi wa Boko Haram, kuna idadi kubwa ya Wakristo na viongozi wao wanaoamini kuwa Waislamu waliowengi ni wapenda amani.
Tokea Boko Haram ianzishe uasi wake Nigeria mwaka 2009, watu elfu 20 wamepoteza maisha. Aidha zaidi ya watu milioni mbili wamefanywa wakimbizi kufuatia ugaidi wa Boko Haram.
Neno Boko Haram kwa lugha ya Kihausa lina
maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram
ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa
likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi
hiyo.