Amri hiyo imetolewa na
mkuu wa Idara ya Viwango vya Elimu Uingereza (Ofsted) ambaye pia ni mkaguzi
mkuu wa shule, Bi. Amanda Spielman. Ametoa uamuzi huo wiki moja tu baada ya
kukutana na wanaofanya kampeni za kupinga hijabu katika shule za Uingereza
ambao walionekana kukasirishwa na ripoti iliyosema asilimia 20 ya shule 800 za
serikali katika maeneo 11 ya England zimeorodhesha hijabu kama sehemu ya mavazi
rasmi ya shule au unifomu, ingawa wenye kuvaa wana hiari.
Kufuatia uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Uingereza, Harun Khan amebainisha wasi wasi wake kwamba Ofsted imetangaza kuwalenga na kuwasaili wasichana wa shule wanovaa mtandio.
"Ujumbe wa wazi hapa kwa wanawake wote Uingereza wanaovaa hijabu ni kuwa wao ni raia wa daraja ya pili, "amesema Khan.
Aidha amebainisha masikitiko yake kuwa hivi sasa kubaguliwa wanaovaa hijabu ni sera nchini Uingereza. Amesema sera kama hivyo itakuwa na matokeo ambayo hayakukusudiwa huku akisisitiza kuwa wazazi Waislamu na watoto wao wana haki ya maamuzi na hawapaswi kupuuzwa
Waislamu ni takriabni asilimia 4.4 ya watu wote Uingereza na ni jamii ya waliowachache inayostawi kwa kasi zaidi.