IQNA

Makaburi ya umati ya Waislamu wa Myanmar yagunduliwa

23:09 - February 02, 2018
Habari ID: 3471378
TEHRAN (IQNA)-Makaburi ya umati ya Waislamu waliouawa nchini Myanmar yamepatikana katika kijiji kimoja katika jimbo la Rakhine magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema maamia ya Waislamu wa jamii ya Rohingaya wanaaminika kuuawa na kisha kuzikwa katika makarubi hayo ambayo yamegunduliwa katika kijiji cha Gu Dar Pyin katika jimbo la Rakhine ambalo wakazi wake wengi ni Waislamu.

Wakimbizi waliokimbilia hifadhi katika nchi jirani ya Bangladesh wamethibitisha kuwa kulijiri mauaji makubwa katika kijiji hicho.

Utawala wa kiimla wa Myanmar umekata mawasiliano yote na kijiji cha Gu Dar Pyin na hivyo wachunguzi hawajaweza kubainisha idaid kamili ya watu waliouawa, hatahivyo picha za satalaiti za shirika la DigitalGlobe zinaonyesha kijiji hicho kiliangamizwa kikamilifu katika oparesheni ya jehsi katili la Myanmar.

Viongozi wa kijamii wameorodesha watu 75 waliothibitishwa kupoteza maisha katika kijiji hicho lakini, wanakijiji wanasema idadi hiyo inaweza kuwa zaidi ya 400 kwa kutogemea ushahidi wa jamaa na miili iliyoonekana imetapakaa katika eneo hilo.

Jinai kubwa wanazofanyiwa Waislamu hao na wanajeshi na Mabudha wa nchi hiyo  wenye misimamo ya kufurutu katika mkoa wa Rakhine magharibi mwa Myanmar zilishika kasi tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu. Hadii sasa  jina hizo zimepelekea kuuliwa Waislamu zaidi ya elfu sita na kujeruhiwa maelfu ya wengine huku wengine karibu laki saba wakilazimika kuwa wakimbizi katika nchi jirani ya Bangladesh.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa uhalifu unaofanywa na Mabudha kwa himaya ya serikali nchini Myanmar dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya ni mauaji ya kimbari.

Zeid Ra'ad Al Hussein anasisitiza kwamba, kuna udharura wa kufika katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na kufanya uchunguzi kuhusu ukatili unaofanywa na serikali ya Myanmar dhidi ya Waislamu.

3465096

captcha