Katika mahojiano na IQNA, Ustadh Adel Mahmoud Khalil amesema mitandao ya kijamii ni teknolojia ya kisasa inayoweza kutumika kwa kiasi kikubwa katika kufundisha usomaji Qur’ani.
Pamoja na hayo Khalil ambaye ni qarii wa Qur’ani na pia hushiriki kama jaji katika mashindano ya kimatiafa ya Qur’ani amesisitiza kuwa mbinu ya jadi ya kufunza Qur’ani katika madrassah au shule, misikiti na halaqah au halqa za Qur’ani bado inapaswa kutumika sambamba na teknoojia za kisasa.
“Hatupaswi kusahau kuwa intaneti na mitandao ya kijamii inatumia na idadi kubwa ya watu duniani, nah ii ni fursa iliyopo ili tuweze kufunza Qur’ani na sayansi zake.”
Ustadh Khalil ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Kufundisha Qur’ani cha Jumuiya ya Qur’ani ya Lebanon anasema kituo hicho kimezindua tovuti ya kufundisha Qur’ani. Tovuti hiyo inatoa mafunzi kuhusu qiraa, Tafsir na sayansi kadhaaa za Qur’ani. Anasema mtu aliye sehemu yoyote duniani anaweza kunufuaika na mafunzo wanaytoa.
Huku akiashiria namna makundi ya wakufurishaji wanavyotumia intaneti kueneza tafsiri potovu za Qur’ani, amesema kuna haja ya wanazuoni wa Kiislamu nao kutumia kila mbinu kueneza mafundisho sahihi ya Kiislamu ili kukabiliana na idiolojia zenye kuwapotosha Waislamu.
Ustadh Khalil amemaliza kwa kuwanasihi Waislamu, hasa vijana, kutekeleza mafundisho ya Qur’ani Tukufu mbali na kuhifadhi na kusoma aya zake.