IQNA

Vikao vya Qur'ani katika kambi za 'Maandamano ya Kurejea' Ghaza

19:36 - May 06, 2018
Habari ID: 3471498
TEHRAN (IQNA) – Wapalestina wameweka kambi maalumu za kusoma Qur'ani katika maeneo ya 'Maandamano ya Kurejea' katika Ukanda wa Ghaza pamoja na kuwa wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamekuwa wakiwafyatulia risasi na kuwaua Wapalestina.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Wapalestina wameweka kambi kadhaa za kusoma Qur'ani Tukufu katika upande wa Ghaza wa mpaka na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na Israel.

Ukatili wa Wazayuni haujawateteresha Wapalestina na wamebakia imara na kuendelea kushiriki katika vikao vya Qur'ani sambamba na maandamano ya kupinga utawala haramu wa Israel. Ustadh Taha Saud, Mpalestina Hafidh wa Qur'ani Tukufu, amesema sauti ya Qur'ani kwa kawaida husikika katika misikiti na vituo vya Qur'ani lakini mara hii sasa wameamua kupata uzoefu mpya. Amesema vikao vya qiraa ya Qur'ani hufanyika kila asubuhi katika kambi hizo za waandamanaji. "Risasi za Waisraeli haziwezi kuvunja azma yetu ya kusoma Qur'ani Tukufu," ameongeza.

Tokea maandamano hayo ya amani ya kila Ijumaa yaanze Machi 30 hadi sasa, Wapalestina wapatao 49 wamekufa shahidi baada ya kufyatuliwa risasi na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel Israel huku wengine zaidi ya 6000 wakijeruhiwa.

Lengo la kufanyika maandamano hayo ni kusisitiza haki ya kurejea Wapalestina katika ardhi zao ambazo ziliporwa na Wazayuni.

Kilele cha maandamano hayo kitakuwa ni katikati ya Mwezi Mei wakati ambao Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza atauhamisha ubalozi wa nchi yake kutoka Tel Aviv hadi mji wa Quds Tukufu (Jerusalem). Maandamano hayo makubwa ya Wapalestina yamekuwa ni pigo kubwa kwa rais wa Marekani na baadhi ya waitifaki wake wahaini katika nchi za Kiarabu ambao wanataka kadhia ya Palestina imalizike kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

 3465736

captcha