IQNA

12:22 - May 08, 2018
News ID: 3471501
KUALA LUMPUR (IQNA)- Mashindano ya 60 ya Kimataifa ya Kuhifadhi na Kusoma Qur'ani Tukufu ya Malaysia yameanza Jumatatu katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Kiislamu kusini mashariki mwa Asia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sherehe za ufunguzi zimefanyika katika Ukumbi wa Putra World Trade Center kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Mashindano ya mwaka huu yana wawakilishi kutoka nchi 56 ambapo kuna vitengo tafauti vya wanawake na wanaume.

Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Jumamosi Mei 12 ambapo washindi watatunukiwa zawadi.

Mwaka jana mashindano hayo yalikuwa na washiriki kutoka nchi 49 ambapo Qari Hamed Alizadeh wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alipata nafasi ya kwanza katika qiraa ya Qur'ani Tukufu.

Miaka miwili kabla, Qarii wa Iran, Shahidi Mohsen Hajihassani Kargar, alifariki katika maafa ya Mina katika Ibada ya Hija mwaka 2015, alishika nafasi ya kwanza katika mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani.

3712331

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Malaysia

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Malaysia

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Malaysia

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani yaanza Malaysia

Name:
Email:
* Comment: