IQNA

23:08 - May 09, 2018
News ID: 3471503
TEHRAN (IQNA)-Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limetoa wito kwa Waislamu kote Marekani kuchukua tahadhari katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Katika taarifa siku ya Jumanne, CAIR imesema kumeshuhudiwa ongezeko la hujuma au vitendo vinavyochochewa na chuki dhidi ya Waislamu tokea Donald Trump ashinde uchaguzi wa rais Marekani mwaka 2016.

Kwa mujibu wa CAIR kutokana na kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani idadi ya Waislamu wanaojumuika katikamisikiti au vitu vya Kiislamu huongezeka, kuna uwezakano mkubwa kuwa watu wenye chuki dhidi ya Waislamu wakawashambulia Waislamu.

Kwa msingio huo Waislamu wametakiwa kuimarisha usalama katika misikiti na vituo vya Kiislamu au sehemu yoyote ile wanayojumuika kwa ajili ya ibada.

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unatazamiwa kuanza Mei 15 nchini Marekani na kumalizika Juni 14.

3465777

Name:
Email:
* Comment: