IQNA

12:32 - May 11, 2018
News ID: 3471505
TEHRAN (IQNA)- Mahakama ya Leba mjini Berlin, Ujerumani imesema baraza la mji lina haki ya kumzuia mwalimu Mwislamu kuvaa Hijabu na hivyo kutupilia mbali malalamiko yake ya kubaguliwa.

Katika hukumu yake siku ya Jumatano, Jaji Arne Boyer, amesema sheria ya mji huo inayojulikana kama 'sheria ya kutopendelea upande wowote' inapiga marufuku nembo na mavazi ya kidini ya wafanyakazi wa umma na hivyo ina nguvu zaidi kuhusu haki ya kuabudu. 

Hukumu hiyo, ambayo itapingwa katika mahakama ya rufaa, inatazamiwa kukithirisha mijadala Ujerumani kuhusu Hijabu ambapo kuna hitilafu za kisheria kuhusu vazi hilo katika majimbo 16 nchini humo.

Sheria ya Ujerumani inawapiga marufuku wafanyakazi wa umma kufunika nyuso zao kwa mavazi kama vile niqabu au burka.

Hatahivyo hakuna marufuku ya kitaifa ya Hijabu ingawa baadhi ya majimbo yamepiga marufuku vazi hilo la staha la mwanamke Mwislamu. Hii ni katika hali ambayo jimbo la Bavaria lenye Wakatoliki wengi hivi karibuni liliamuru misalaba iwekwe katika milango yote ya majengo ya serikali. Tayari shule na mahakama za jimbo hilo huwa zina misalaba katika maeneo maalumu.

3465785

Name:
Email:
* Comment: