IQNA

17:37 - May 21, 2018
News ID: 3471524
TEHRAN (IQNA) Mkuu wa Halmasahuri ya Mapatano Uganda (URA) amekanusha taarifa kuhusu kuwepo mpango wa kutoza ushuru nakala za Qur'ani Tukufu na Bibilia.

Doris Akol Kamishna Mkuu wa URA amekanusha taarifa za vyombo ya habari kuhusu uamuzi wa kuanza kutoza kodi vitabu hivyo vitakatifu. Huku akizitaja ripoti hizo kuwa bandia, amesema na kuongeza kuwa kinyume cha habari hizo kuna marekebisho ya sheria kwa lengo la kuhakikisha kuwa nakala za Qur'ani na Bibilia hazitozwi ushuru.

Awali Ramadhan Mugalu, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu nchini Uganda alimtaka Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo kutekeleza ahadi aliyoitoa ya kutovitoza ushuru vitabu vya kidini vinavyoingia nchini humo.

Amesema, "Serikali imevuka mipaka sasa katika jitiada zake za kukusanya ushuru. Itawezekanaje kutoza kodi Neno la Mungu? Badala yake inapaswa kusaidia katika juhudi za kuchapishwa vitavu hivyo nchini."

Naye Joshua Kitakule, Katibu Mkuu wa Baraza la Muungano wa Kidini nchini humo amesema, "Vitabu hivyo haviingizwi nchini kwa ajiili ya kupata faida, na hata iwapo serikali lazima itoze ushuru vitabu hivyo, hicho kiwango cha asilimia 18 ni cha juu mno."

3715283

Name:
Email:
* Comment: