IQNA

15:07 - August 26, 2018
News ID: 3471647
ISLAMABAD (IQNA)- Kozi ya misingi ya Tajwidi katika kusoma Qur'ani Tukufu inafanyika nchini Pakistan kwa kutumia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, kozi hiyo ambayo ilianza Ijumaa inatazamiwa kuendelea hadi Septemba 6.

Akademia ya Qurani na Itrat nchini Pakistan imesema iandaa kozi hiyo kwa lengo la kueneza mafundisho ya Qur'ani Tukufu. Aidha lengo jingine la kozi hiyo ni kuwasaidai washiriki kuimarisha uwezo wao wa kusoma Qur'an TUkufu.

Waislamu kote duniani ambao wanazungumza lugha ya Kiurdu wanaweza kushiriki katika kozi hiyo kwa njia ya WhatsApp kupitia nambari ya +923312413113.

3741342

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: