IQNA

Kinara wa magaidi wa ISIS nchini Mali auawa

13:53 - August 28, 2018
Habari ID: 3471650
TEHRAN (IQNA)- Kinara wa kundi la kigaidi linalofugamna na ISIS au Daesh nchini Mali ameuawa katika mapigano.

Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imedai kuwa wanajeshi wake Jumapili walimuua kinara huyo wa ISIS aliyetambuliwa kwa jina la Mohamed Ag Almouner ambaye alikuwa mkuu wa kundi la ISIS katika Sahara Kubwa (ISGS).

Aidha wizara hiyo imesema raia wengine wawili akiwemo mwanamke walipoteza maisha katika oparesheni hiyo.

Ufaransa ina wanajeshi  4,000 katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi kama sehemu ya oparesheni inayodaiwa ni ya kupambana na magaidi.

Kundi la ISIS katika Sahara Kubwa (ISGS) linaendesha harakati zake nchini Mali na kamanda wake mkuu ametajwa kuwa Adnan Abu Walid Sahrawi ambaye alikuwa kuwa mwanachama wa Kundi la Al Qaeda katika eneo la Maghreb (AQIM).

Tangu mwaka 2012 Mali imekuwa ikishuhudia machafuko baada ya makundi ya kigaidi kuyakalia baadhi ya maeneo ya ardhi ya nchi hiyo.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kulinda amani nchini Mali (MINUSMA) na askari wa jeshi la Ufaransa walitumwa nchini humo tangu katikati ya mwaka 2013, lakini wameshindwa kurejesha amani na uthabiti na tishio la ugaidi lingali linahatarisha usalama wa nchi hiyo.

3466632

captcha