IQNA

Misri haitawaruhusu wenye misimamo mikali ya kidini kuanzisha vituo vya Qur’ani

13:41 - October 28, 2018
Habari ID: 3471722
TEHRAN (IQNA)-Waziri wa Wakfu nchini Misri amesema wizara yake haitaruhusu makundi yenye misimamo mikali ya kidini kuanzisha vituo vya kuhifadhi Qur’ani nchini humo.

Akizungumza hivi karibini katika Jimbo la Suez, Sheikh Mohammad Mokhtar Gomaa amesema watu wanaofungamana na makundi yenye misimamo mikali ambao wamepigwa marufuku kuhubiri misikitini sasa wanatumia mbinu ya kuanzisha shule za chekechea na vituo vya kuhifadhi Qur’ani kwa lengo la kuwaathiri watoto kwa itikadi zenye kufurutu ada.

Waziri Gomaa amesisitiza kuwa vituo vya kuhifadhi Qur’ani vilivyopata vibali vya Wizara ya Wakfu ndivyo pekee vitakavyoruhusia kuendesha shughuli zao.

Serikali ya Misri inasema Harakati ya Ikhwanul Muslimin kuwa yenye misimamo mikali ya kidini na hivyo imepigwa marufuku.

Kwingineko Sheikh Gomaa amesema mwaka jana wizara yake ilianzisha vituyo 764 vipya vya kuhifadhi Qur’ani na hivyo kuongeza idadi jumla ya vituo hivyo kuwa 1,500 kote Misri.

3758977

captcha