IQNA

Saudi Arabia yalaaniwa kwa kuwanyonga watu kwa ajili ya itikadi zao

23:30 - April 24, 2019
Habari ID: 3471928
TEHRAN (IQNA)- Saudi Arabia inaendelea kulaaniwa kimataifa kw akuwanyonga raia wan chi hiyo kutokana na itikadi zao zinazokinzana na zile za watawala wa ukoo wa Aal Saud.

Jana Jumanne, utawala wa kiimla wa  Saudi Arabia uiwanyonga kwa kuwakata vichwa watu 37, ambapo 32 miongoni  mwao walikuwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Idadi hiyo ya walionyongwa ni kubwa zaidi baada ya kunyongwa raia wengine waa nchi hiyo mwaka 2016 akiwemo mwanazuoni maarufu wa Kiislamu wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr Baqir al Nimr.

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International limekosoa vikali kitendo cha utawala wa Aal-Saud cha kutekeleza hukumu ya kuwanyonga makumi ya Waislamu wa Kishia nchini Saudi Arabia, likisisitiza kuwa utawala huo wa kifalme hauheshimu thamani ya utu.

Mkurugenzi wa Utafiti wa shirika hilo katika eneo la Asia Magharibi, Lynn Maalouf amelaani vikali hatua ya watawala wa Riyadh kutumia kisingizio cha kupambana na ugaidi kuwanyonga kwa umati Waislamu wa Kishia.

Amnesty International imesema ni jambo la kusitikisha namna Riyadh inavyotumia 'Sheria ya Kupambana na Ugaidi' kuwabinya na kuwakandamiza Waislamu hao ambao ni katika jamii ya walio wachache nchini humo.

Wakati huo huo, afisa mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaani vikali hatua ya Saudi kuwanyinga wanaume 37 katika miji sita tafauti nchini humo. Amesema mkondo wa sheria haujafuatwa na kesi zilizosikilizwa zilikiuka taratibu huku baadhi wakilazimika kukiri makosa ambayo hawajafanya baada ya kuteswa.

Umoja wa Ulaya nao umetoa taarifa na kulaani hatua hiyo ya Saudia kuwanyonga bila kuwepo uadilifu katika mfumo wa mahakama.

Jumuiya ya Maulamaa wa Yemen nayo imepaza sauti na kulaani hatua ya Saudi kuwanyonga watu wasio na hatia. Harakati ya Hizbullah ya Lebanon nayo pia imetoaa taarifa na kulaani hatua hiyo ya Saudia kuwanyonga kwa umati watu wasio na hatua na sambamba na kubainisha kufungamana na familia za mashahidi wa ukatili huo, imetUma salamu za rambI rambi kumuomba Mwenyezi Mungu azipe familia za waathirika subira.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa wakati Saudia inapowanyonga watu 37 rais Trump wa Marekani hasemi chochote. Ameongeza wale wote walio katika Timu B yaani Bolton, Bin Salman, Bin Zaye na Benjamin Netanyahu, wanapotenda jinai hupata kinga.

3806345

Kishikizo: iqna saudi arabia
captcha