IQNA

Saudia kubomoa msikiti eneo la Qatif, Waislamu walalamika

20:48 - December 01, 2020
Habari ID: 3473410
TEHRAN (IQNA)- Utawala wa kifalme wa Saudi Arabia umetoa amri ya kubomolewa msikiti alimokuwa akiswalisha mwanazuoni maarufu wa Waislamu wa madehehebu ya Shia, Shahidi Sheikh Nimr Baqir al-Nimr.

Kwa mujibu wa taarifa, Msikiti wa Imam Hussein (AS) katika eneo la Qatif mashariki mwa Saudia utabomolewa kwa kisingizio cha kutoa nafasi kwa ajili ya ‘miradi ya maendeleo’.

Mwanaharakati wa haki za binaadamu Saudia, Adel al-Saeed amesema lengo la kubomolewa msikiti huo ni kuondoa athari zote zinazowakumbusha Waislamu kuhusu mwanazuoni huyo aliyeuawa shahidi.

Waislamu katika eneo la Qatif wanalalmikia vikali kitendo hicho lakini vilio vyao vimepuuzwa kabisa na watawala wa ukoo wa Aal Saud. Adel al-Saeed amesema hata wakuu wa Saudia wakiubomoa msikiti huo, kumbukumbu ya Sheikh al-Nimr daima itabaki katika nyoyo za Waislamu.

Sheikh Nimr aliuawa shahidi kwa kunyongwa  Januari 2, 2016 kufuatia amri ya mahakama ya kidhalimu ya Saudia.

Sheikh Nimr alikamatwa mwaka 2012 kwa kutoa hotuba ambazo zilikuwa zinaukosoa vikali utawala dhalimu na wa kifisahdi wa Saudia. Utawala wa kiimla wa Saudia ulikosolewa vikali kwa kitendo hicho cha kidhalimu cha kumnyonga mwanazuoni huyo maarufu wa Kiislamu.

3938583

captcha