IQNA

Nchi 90 kushirki Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai

10:17 - April 27, 2019
Habari ID: 3471930
TEHRAN (IQNA)- Wawakilishi wa nchi 90 wanatazamiwa kushiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Dubai.

Hayo yametangazwa na mkuu wa kamati andalizi ya mashindano hayo, ambayo pia yanajulikana kama Zawadi ya Qur'ani ya Dubai, Ibrahim Bu Melha ambaye amesema kuna uwezekano pia idadi hiyo ikafika 100.
Ameongeza kuwa kinyume na miaka ya nyuma wakati mashindano hayo yalianza katika wiki ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, mwaka huu mashindano hayo yataanza katika siku ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kwa muda wa siku 12. Aidha amesema majaji wa mashindano hayo mwaka huu watakuwa ni wataalamu wa Qur'ani kutoka mwenyeji, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Saudi Arabia, Algeria, Libya na Burkina Faso.

3806500

captcha