Hakuna njia nyingine ya kuelewa njia ya ukamilifu zaidi ya kukimbilia Qur’ani Tukufu, Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi alisema, alipohutubu kwenye hafla ya kufunga Mashindano ya 47 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran huko Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran siku ya Alhamisi.
Akisisitiza umuhimu wa Qur’ani, alinukuu Aya ya 21 ya Surah Al-Hashr, “Lau kuwa tumeiteremsha hii Qur´ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeli uona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri.”
Ameongeza kuwa Qur’ani Tukufu inatoa kielelezo kamilifu, yaani Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ili sisi tufikie ukamilifu.
Mtume (SAW) ni kigezo bora kwa wale wanaomuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Kiyama, amesisitiza na kuongeza kwamba ni lazima tuelekee katika Qur'ani ili tufikie ukamilifu kuwa jambo la kweli, na kwamba katika suala hili, ni muhimu kwa nyumba na jumuiya zetu kujumuisha maadili ya Qur'ani na Fatimi akiashiria Bintiye Mtume Muhammad (SAW), Bibi Fatima Zahra (SA)
Kwingineko katika matamshi yake, Hujjatul Islam Khamoushi alisema kuwa Shirika la Wakfu, ambalo huandaa mashindano ya Qur'ani kila mwaka, hutumikia Qur'ani.
Duru ya mwisho ya shindano hilo katika kategoria tofauti kwa upande wa wanaume ilihitimishwa Jumatano, na washindi walitangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga leo.
4255052