IQNA

11:42 - May 05, 2019
News ID: 3471941
TEHRAN (IQNA)-Misikiti katika eneo la Long Island mjini New York nchini Marekani imeimarisha usalama kwa kuwaajiri walinzi wenye silaha katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuatia hujuma za hivi karibuni za kigaidi katika maeneo ya ibada kote duniani.

Misikiti 10 kati ya 30 katika eneo hilo, lenye Waislamu karibu 80,000, imeimarisha usalama katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na wasi wasi uliopo.

Nayyar Imam, kiongozi wa Muungano wa Waislamu wa Long Island amesema ni jambo la kusikitisha kuwa katika zama hizo nchini Marekani tunalazimika kuwa na walinzi wenye silaha wakati wa kuswali. Amesema hawana budi ila kuchukua hatua hizo kali la usalama ili kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea.

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, mamia ya wafuasi wa duni za Kiislamu, Kikristo na Kiyahudi, wameuawa katika hujuma dhidi ya maeneo yao ya ibada nchini New Zealand, Sri Lanka na Marekani.

Wimbi la hujuma hizo lilianza Machi 15 wakati Waislamu 51 waliuawa kwa kupigwa risasi katika hujuma ya kigaidi iliyolenga waumini katika misikiti miwili huko mjini Christchurch New Zealand. Wiki tano baadaya katika Jumapili ya Pasaka, magaidi wa kundi la ISIS walilenga makanisa matatu na hoteli tatu za kifahari  katika mji mkuu wa Sri Lanka, Colombo na kuwaua watu zaidi ya 257. Magaidi pia walihujumu makanisa na mahoteli katika maeneo ya Negombo na  Batticaloa nchini humo.  Siku kadhaa baada ya tukio hilo mtu aliyekuwa na silaha alishambulia sinagogi huko San Diego Marekani na kuua mwanamke na kumjeruhu kuhani. Gaidi aliyedai kuhusika na hujuma hiyo ni mwanachama pote la Wakristo Walokole na alidai pia kuhusika katika kuuteketeza moto msikiti katika eneo hilo.

/3468436

Name:
Email:
* Comment: