IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
12:09 - May 09, 2019
News ID: 3471949
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha majukumu ya Hawza (vyuo vikuu vya kidini) na maulamaa katika kubainisha maarifa ya Uislamu na kufanya juhudi kwa ajili ya kufikiwa hilo katika jamii na kusisitiza kwamba, maulamaa wakiwa warithi wa Manabii wanapaswa kufanya hima kubwa ili tawhidi na uadilifu vipatikane kivitendo katika jamii.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema hayo jana katika siku ya pili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wakati alipokutana hapa mjini Tehran na kundi la matalaba (wanafunzi wa masomo ya dini), walimu, masheikh na wakurugenzi wa vyuo vya kidini wapatao 2,000 kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini na kubainisha majukumu makubwa waliyonayo wahusika katika kubainisha maarifa ya Uislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria mahitaji ya leo ya wanadamu kwa maarifa ya dini na kupokewa maarifa hayo katika Ulimwengu wa Kiislamu na hata nje ya Ulimwengu wa Kiislamu na kusisitiza kwamba, jukumu la vyuo vya kidini ni zito na kubwa hii leo kuliko huko nyuma.

Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa, uzingatiaji wa leo wa masuala ya kidini na kiroho uliopo ndani ya nchi hauwezi kulinganishwa na huko nyuma na kabla ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aidha amesema kuwa, vyuo vya kidini ni kituo cha mafundisho ya Uislamu na kuongeza kuwa, kuwafahamisha na kuwafundisha watu maarifa ya kidini ni sehemu ya majukumu ya vyuo vya kidini na sehemu nyingine ya jukumu hili ni kuhakikisha kwamba, maarifa haya ya kidini yanadhihirika na kuonekana katika maisha ya umma.

3468472

Name:
Email:
* Comment: