IQNA

20:23 - May 12, 2019
News ID: 3471953
TEHRAN (IQNA)- Waziri wa Wakfu huko Misri ametangaza kuwa misikiti 300 itafunguliwa nchini humo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa, Mohammad Mokhtar Goma, Waziri wa Wakfui Misri nchini Misri ameyasema hayo hivi karibuni wakati wa kufunguliwa Msikiti wa Jamia wa Ahmad Urabi katika mji wa Hirriyat Razan karibu na Zagazig mkoani Sharqia.

Sheikh Mohammad Al Awzi, mwanachama wa Kamati ya Ujenzi wa Misikiti Misri amesema ukarabati wa Msikiti wa Ahmad Arabi umegharimu pauni za Misri milioni 15.

Akihutubu katika hafla hiyo Waziri Mokhtar Goma amesema misikiti 300 itafunguliwa kote nchini humo katika siku za awali za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Amesema kufunguliwa idadi hiyo ya misikiti katika kipindi cha wiki moja ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa katika historia ya Misri na dunia.

3808142

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: