IQNA

11:03 - May 22, 2019
News ID: 3471968
TEHRAN (IQNA)- Gaidi raia wa Australia aliyefanya mauaji ya umati dhidi ya Waislamu katika mji wa Christchurch huko New Zealand amefikishwa kizimbani kujibu mashtaka.

Jeshi la Polisi nchini New Zealand limesema mbali na mashtaka ya ugaidi, gaidi huyo pia anakabiliwa na mashtaka mengine kadhaa. Mashambulizi yaliyofanywa katika misikiti miwili ya mji wa Christchurch nchini News Zealand Machi 15 yalipelekea Waislamu 51 kuuawa shahidi na makumi ya wengine kujeruhiwa.

Gaidi Brenton Tarrant mwenye misimamo mikali ya kibaguzi ya rais wa Marekani, Donald Trump anakabiliwa pia na mashtaka mengine 51 ya mauaji na mashtaka mengine 40 ya kujaribu kuua.

Kesi ya gaidi huyo imepangwa kusikilizwa tena mwezi ujao wa Juni 14. Katika hujuma hiyo iliyojiri wakati wa Sala ya Ijumaa, gaidi huyo mwenye chuki dhidi ya Uislamu ambaye alitangaza mwenyewe kuwa ni mfuasi wa Trump, aliyarusha hewani mubashara mauaji hayo ya kinyama kupitia facebook na Youtube. Wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo ya kinyama ambayo iliutikisa ulimwengu mzima.

3468581

 

Name:
Email:
* Comment: