IQNA

17:42 - August 04, 2019
News ID: 3472070
TEHRAN (IQNA)- Kwa akali watu 20 wameuawa na wengine 24 kujeruhiwa kufuatia tukio la hujuma ya kigaidi lililotokea leo Jumapili katika jimbo la Texas nchini Marekani.

Taarifa zinasema aliyetekeleza hujuma hiyo ni mzungu mwenye misimamo mikali ya kibaguzi ambaye aliunga mkono wazi wazi mauaji ya Waislamu katika Sala ya Ijumaa huko Christchurch New Zealand mwezi Machi mwaka huu. Hujuma hiyo ya kigaidi iliyopelekea Waislamu zaidi ya 50 kuuawa nayo pia ilitekelezwa na mzungu mwenye misimamo mikali na muungaji mkono sugu wa Rais Donald Trump wa Marekani.
Tukio la Texas ambalo ni mlolongo wa matukio ya mauaji kama hayo nchini Marekani limetokea katika eneo moja lenye maduka la Walmart katika mji wa El-Paso. Polisi wanasema wamemkatamata Patrick Crusius kijana mwenye umri wa miaka 21 anayetuhumiwa kuhusika na shambulio hilo.
Kijana huyo baada ya kutiwa mbaroni amesema kuwa, ametekeleza shambulio hilo kutokana na wahajiri wengi kuingia Texas wakitokea Mexico.
Taarifa za awali zinasema kuwa, shambulio hilo linatokana na chuki dhidi ya wahajiri, sera ambazo zimekuwa zikipigiwa debe na Rais Donald Trump wa Marekani.
Wakati huo huo, watu tisa wameuawa kufuatia shambulizi la risasi katika mji wa Dayton, Ohio nchini Marekani. Polisi wamesema hayo mapema leo Jumapili kupitia ukurasa wao wa Twitter na kuongeza kuwa mshambuliaj ni miongoni mwa waliokufa. Watu wasiopungua 16 wamejeruhiwa na wamepelekwa katika hospitali mbaimbali kwa matibabu. Shambulizi hilo linajiri katika muda wa saa 24, baada ya kutokea mkasa mwengine kama huo ambapo watu 20 waliuawa na 26 kujeruhiwa kwa kufyatuliwa risasi na mtu aliyekuwa na bunduki ndani ya duka moja kubwa eneo la El Paso, Texas.
Matukio ya ufyatuaji risasi nchini Marekani hutokea mara kwa mara katika miji na majimbo tofauti ya nchi hiyo.

3469110

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: