IQNA

12:47 - July 13, 2019
News ID: 3472041
TEHRAN (IQNA) -Watu 26 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia shambulio la kigaidi dhidi ya hoteli moja kusini mwa Somalia.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, waandishi wawili wa habari ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la kigaidi Ijumaa mchana katika mji wa Bandari wa Kismayo.
Waandishi habari walipoteza maisha katika hujuma hiyo ya kigaidi mwandishi wa runinga mwenye uraia pacha wa Somalia na Canada Hodan Nalayeh ambapo mume wake pia amepoteza maisha katika hujuma hiyo
Duru zinadokeza kuwa gaidi aligongesha gari lililojaa vilipuzi katika Hoteli ya Medina katika bandari ya Kismayo kabla ya washambuliaji hao kuvamia jengo hilo.
Mashuhuda wanasema kuwa, walisikia milio ya risasi baada ya bomu lililokuwa ndani ya gari hilo kulipuka. Waziri mmoja wa utawala wa eneo hilo pamoja na wakili ni miongoni mwa waliofariki dunia katika shambulio hilo. Maafisa wa usalama wa Somalia wamepambana na magaidi  ndani ya hoteli hadi Jumamosi asubuhi.

Kwa mujib wa Ahmed Mohamed Islam, rais wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Jubaland, raia kadhaa wa kigeni ni miongoni mwa waliouawa katika hujuma hiyo iliyolenga. Amesema raia watatu wa Kenya, watatu wa Tanzania, Wamarekani wawili, Muingereza na Mcanada ni miongoni mwa watu 26 waliouawa katika hujuma hiyo. Rais watatu wa China ni miongoni mwa makumi waliojeruhiwa katika shambulizi hilo la kigaidi.
Magaidi wakufurishaji wa al-Shabab wametangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusika na shambulio hilo.
Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1992 na katika miaka ya hivi hivi karibuni nchi hiyo imeshuhudia kushadidi hujuma za magaidi wa al-Shabab na hivyo kuwasababishia raia wa nchi hiyo matatizo makubwa.
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika maarufu kama AMISOM wanaokadiriwa kufikia 21,000 wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007 ili kujaribu kukabiliana na magaidi wa al-Shabab. Hatahivyo pamoja na vitihada hizo za kimataifa, magaidi wa al-Shabab wanaendelea kutekeelza hujuma Somalia na nchi jirani ya Kenya.

3468939

Name:
Email:
* Comment: