IQNA

10:54 - February 02, 2020
News ID: 3472431
TEHRAN (IQNA) – Msomi nchini Afrika Kusini amesema jamii barani Afrika zina nafasi muhimu katika kukabiliana na misimamo mikali ya kidini kwani serikali pekee haziwezi kukabiliana na tatizo hilo.

Katika mahojiano maalumu na IQNA, Akinola Olojo, mtafiti kuhusu uhalifu wa kimataifa katika Taasisi ya Utafiti kuhusu Usalama, mjini Pretoria Afrika Kusini amesema: "Jamii za Waislamu zinapaswa kuwa angalifu hasa katika nchi ambazo zimeathiriwa makundi yenye misimamo mikali ya kidini ambayo yanatumia vibaya mafundisho ya Kiislamu."

Amesema kuenea makundi ya kigaidi yanayofungamana na ISIS (Daesh) barani Afrika, hasa magharibi mwa bara hilo kunatokanana na udhaifu wa serikali. Ameongeza kuwa, serikali za maeneo ya Afrika Magharibi na Afrika Mashariki zinategemea zaidi nguvu za kijeshi kukabiliana na makundi ya kigaidi katika hali ambayo tatizo ambalo limepelekea kuibuka makundi hayo haliwezi kutatuliwa kijeshi tu. 

Oloji amesema makundi ya kigaidi Afrika yameibuka kutokana na udhaifu wa miongo kadhaa wa serikali za Afrika hasa kutengwa kiuchumi jamii ambazo magaidi hao wameibukia. Halikadhlika amesema serikali za Afrika  zimeshindwa kubuni nafasi za ajira kwa vijana ambao wanazidi kuongezeka katika nchi za Afrika jambo ambalo limetoa mwanya kwa makundi ya kigaidi kujipenyeza na kuwatumia vibaya vijana kwa kuchochea hisia zao za kidini.

Msomo huyo ametoa wito kwa serikali za Afrika kuchukua hatua za haraka kutatuai matatizo ya kiuchumi na uongozi katika jamii ambazo magaidi hubukia. Aidha ametoa wito kwa wasomi wa Kiislamu kujitahidi katika kubainisha mafunzo sahihi ya Uislamu ili kukabiliana na wale wanaoeneza itikadi potovu za kidini. Halikadhalika amesema kuna haja ya kuimarishwa vyombo vya usalama na usimamizi wa mipaka ili kuzuia kuenea makundi ya kigaidi.

Makundi ya kigaidi yanayopata himaya ya Saudia kama vile ISIS  au Daesh, Al Qaeda yana matawi yao kama vile Ansari Sharia ya kaskazini na magharibi mwa Afrika, Boko Haram ya Magharibi mwa Afrika, Al Shabab ya Afrika Mashariki n.k. na ni hatari kubwa kwa usalama wa bara Afrika na dunia nzima.

3470495

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: