IQNA

12:41 - September 03, 2019
News ID: 3472111
TEHRAN (IQNA) – Wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel wamebomoa msikiti wa Wapalestina katika mji wa al Khalil eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Walioshuhudia wanasema mabuldoza ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel mapema Jumatatu yalihujumu mtaa wa Jabal Juhar mjini al-Khalil na kubomoa msikiti uluokuwa ukijengwa hapo.

Kwa mujibu wa Jamal Abu Aram, mkuu wa Idara ya Wakfu ya Al Khalil amesema wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameubomoa msikiti huo bila kutoa tahadhari yoyote.

Aidha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wamebomoa nyumba ya makai ya raia katika eneo hilo kwa kisingizo kuwa haikuwa na kibali cha ujezni.

Idara ya Wakfu Palestina imelaani vikali kitendo hicho cha Israel kuharibu msikiti na kusema hiyo ni hujuma ya wazi dhidi ya matukufu ya Kiislamu na ukikwaji wa wazi wa haki za Waislamu kuabudu.

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kujenga vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu.

Ujenzi huo unaendelea licha ya kwamba tarehe 23 Disemba mwaka 2016 Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio nambari 2334 lililoutaka utawala ghasibu wa Israel kusitisha mara moja na kikamilifu shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi-Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Hata hivyo Israel imepuuza azimio hilo na kuendeleza ujenzi huo kwa himaya na misaada ya Marekani.

3839490

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: