IQNA

11:00 - February 13, 2020
News ID: 3472468
TEHRAN (IQNA) - Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza orodha ya mashirika ambayo yanashirikiana na utawala wa Israel katika kujenga vitongoji haramu katika ardhi za Palestina huko Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Katika taarifa Jumatano, Umoja wa Mataifa umetangaza kuorodhesha majina ya mashirika 112 ya kibiashara  ambayo yanashirikiana na Israel katika kujenga vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni. Kati ya mashirika hayo, 94 yako Israel na  yaliyosalia yako Ufaransa, Marekani, Uholanzi, Luxembourg, Thailand na Uingereza. Taarifa hiyo ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema shughuli za mashirika hayo zinaibua wasiwasi wa ukiukwaji wa haki za binadamu.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatambua kuwa kadhia hiyo imekuwa na utata na itaendelea kuwa na utata.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Palestina Riyad al-Maliki amepongeza ripoti hiyo na kuitaja kuwa ni ushindi kwa sheria za kimataifa. Ametoa wito kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa kuagiza mashirika hayo yasitisha mara moja shughuli zao katika vitongoji vya walowezi wa Kizayuni.

Ni vyema kuashiria pia kuwa tarehe 23 Disemba 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio namba 2334 ambalo liliutaka utawala khabithi wa Kizayuni ukomeshe mara moja shughuli zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Hata hivyo utawala huo umeendelea kukaidi kukiuka azimio hilo sambamba na kuendeleza ujenzi wa vitongoji kwa lengo la kubadili muundo wa maeneo ya Palestina na kuyafanya kuwa miliki yake. Utawala wa Kizayuni wa Israel unapata kiburi cha kukiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa kutokana na kuungaji mkono wa Marekani na tawala vibaraza katika nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saudia Arabia ambazo zimeamua kuwasaliti Wapalestina.

3878508

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: