IQNA

17:26 - November 03, 2019
News ID: 3472198
TEHRAN (IQNA) – Tarjuma ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kilatini imeonyeshwa katika Maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Vitabu (SIBF) huko Sharjah katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Hugo Wetscherek  kutoka taasisi ya Antiquariat Inlibiris ya Austria amesema nakala iliyopo ya tarjuma ya Qur'ani kwa lugha ya Kilatini iliandikwa kwa kutegemea Nakala ya Qurani Tukufu waliyokuwa nayo Pierre de Cluny na Bernard de Clair Vaux huko Toledo, Uhispania katika karbe ya 12 Miladia. Ameongeza kuwa, "De Cluny alimpa Muingereza Robert wa Ketton jukumu la kutarjumu Qur'ani kwa lugha ya Kilatini na alimaliza kazi hiyo mwaka 1143."

Wetscherek anasema tarjuma hiyo ya Qur'ani ya Robert wa Ketton ilimilikiwa na Martin Luther baada ya miaka 400 ambaye alimuamuru Theodore Bibliander aihariri na kuichapisha: "Ingawa tarjuma hiyo ina makosa mengi lakini iliwawezesha wasomi wa nchi za Magharibi kuwa na nakala ya Qur'ani ambayo waliitumia kwa muda mrefu kama marejeo ya kufanya utafiti kuhusu Qur'ani na utamaduni wa Kiislamu."

Aidha katika maonyesho hayo kunaonyeshwa nakala nadra ya Bibilia kwa lugha ya Kiarabu. Nakala hizo zote mbili asili  ziko katika kibanda cha Antiquariat Inlibris cha maonyesho hayo ya vitabu.

3469789

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: