IQNA

13:22 - December 09, 2019
News ID: 3472263
TEHRAN (IQNA) - Daktari wa Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Nigeria Sheikh Ibrahim Zakzaky amesema kuwa msomi huyo ameathiriwa na sumu na anapaswa kupewa matibabu haraka iwezekanavyo.

Nasser Umar Safir amesisitiza kuwa kuendelea kuwepo hai Sheikh Zakzaky licha ya hali yake mbaya ya kiafya ni jambo linalofanana na muujiza.

Daktari Nasser Umar amewaambia waandishi habari jana Jumapili mjini Tehran kwamba, tangu mwezi Disemba mwaka 2015 baada ya Husseiniya ya Baqiyyatullah kushambuliwa na jeshi la Nigeria katika mji wa Zaria afya ya Sheikh Zakzaky inaendelea kuzorota sana na iliamuliwa kuwa apelekwe nchini India kwa ajili ya matibabu lakini serikali ya Abuja ilitatiza mchakazo wa kupewa matibabu kwanazuoni huyo wa Kiislamu na akarejeshwa jela huko Nigeria.

Daktari wa Sheikh Zakzaky ameashiria hali na mazingira mabaya ya jela anakoshikiliwa kiongozi huyo na kusema: "Tumeshuhudia kwa macho unyanyasaji na ukatili mkubwa unaofanyika katika jela hiyo na wenzangu wanne wameuwa katika jela hilo."

Daktari Nasser Umar amesema kuwa, baada ya kuchunguza mwili na afya Sheikh Zakzaky imebainika kuwa, ameathiriwa na kemikali na sumu iliyotokana na zana na vyombo vinavyotumiwa katika jela hiyo.  

Akitoa vielelezo na picha za maeneo mbalimbali ya mwili wa Zakzaky, daktari huyo amesema kuwa, fuvu la kichwa cha Sheikh Zakzaky limepatikana na mipasuko 43 na kwamba kuendelea kuwa hai kwa mwanazuoni huyo licha ya matatizo yake makubwa ya kiafya na ukatili aliofanyika ni sawa na muujiza.

Bintiye Sheikh Zakzaky pia amehutubia mkutano wa waandishi habari na ametoa wito kwa serikali ya Nigeria kuwaachili huru wazazi wake baada ya kuwashikilia kwa muda wa miaka minne kwa tuhuma bandia. Bi. Suhaila Zakzaky amesema serikali ya Nigeria aidha amebainisha wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya ya wazazi wake yako hatarini.

Siku chache zilizopita Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna nchini Nigeria ilikubali ombi la gavana wa jimbo hilo la kupelekwa kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe katika jela kuu ya jimbo hilo.

Itakumbukwa kuwa tarehe 13 Disemba 2015, jeshi la Nigeria lilifanya mauaji ya kikatili dhidi ya Waislamu wa Nigeria baada ya kuivamia Husainia ya mji wa Zaria na kumteka nyara Sheikh Zakzaky baada ya kumpiga risasi kadhaa.

3470060

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: