IQNA

10:11 - December 16, 2019
News ID: 3472281
TEHRAN (IQNA) – Mkutano wa Saba wa Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) umefanyika wiki hii katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Kongamano hilo la siku mbili limefanyika kuanzia Disemba 15-17 2019 na kuwaleta pamoja mawaziri wa afya kutoka zaidi ya nchi 40 za Kiislamu. Aidha wawakilishi wa taasisi za OIC na za kimataifa, wameshiriki katika mkutano huo. 

Miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo ni  Katibu Mkuu wa OIC Dkt. Youssef bin Ahmed Al-Uthaymeen, Secretary-General of the Organization of Islamic Cooperation, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Daktari Tidros Gebresos.

Mkutano huo umejadili kuhusu njia za kuboresha afya katika nchi za Kiislamu kwa kushirikiana na jamii ya kimataifa. Kati ya mada muhimu zilizojadiliwa ni pamoja na kuimarisha mfumo wa afya, kuzuia magonjwa, afya ya mama mzazi na mtoto, lishe, dawa, chanjo, teknolojia za kitiba, huduma za kiafya za dharura, utafiti na elimu.

3470115

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: