IQNA

Umrah 1446

Wanaoenda Umrah wahimizwa kufuata Itifaki za Afya

23:21 - August 28, 2024
Habari ID: 3479340
IQNA - Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi imetoa taarifa ikitambulisha kanuni mpya za Hija ndogo ya Umrah.

Katika taarifa hiyo, wizara ilisisitiza haja ya wanaoshiriki  Umrah kuzingatia itifaki za afya.

Pia ilisisitiza umuhimu wa kuvaa barakoa kwa ajili ya kuzuia kuenea kwa virusi na magonjwa ya kupumua ya kuambukiza.

Ikizingatiwa kuwa kuna mikusanyiko mikubwa na umati katika maeneo matakatifu wakati wa ibada ya Umrah, kuvaa barakoa husaidia sana katika kulinda afya za wanaoshiriki katika Hija hiyo ndogo taarifa hiyo ilisoma.

Wanaoshiriki halikadhalika wanatakiwa kuzingatia umbali wa kijamii  au kutokaribiana ili kupunguza hatari ya kuenea kwa virusi.

Pia wanahimizwa kunawa mikono kwa maji na sabuni na kutumia dawa za kuua vijidudu, kulingana na taarifa hiyo.

Umrah ni safari ya kwenda kwenye mji mtakatifu wa Makka na Waislamu wanaweza kutekeleza ibada hiyo  wakati wowote wa mwaka, tofauti na Hija ambayo inaweza kufanywa tu katika siku za kwanza za mwezi wa Hijri wa Dhul Hajja.

 

4233705

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: umrah Afya
captcha