IQNA

Rais Rouhani asema Ulimwengu wa Kiislamu una uwezo mkubwa

12:50 - December 17, 2019
Habari ID: 3472284
TEHRAN (IQNA) - Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa sera za kueleka mashariki na kuwa na uhusiano wa karibu zaidi na nchi muhimu za bara Asia ni miongoni mwa malengo ya siku zote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Rais Rouhani ameyasema hayo mapema leo kabla ya kuondoka mjini Tehran akielekea Malaysia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kimataifa wa Kuala Lumpur 2019. Amesema kuwa, mkutano huo utajadili uhusiano wa pande kadhaa katika Ulimwengu wa Kiislamu.

Vilevile ameashiria uwezo wa Ulimwengu wa Kiislamu katika masuala mbalimbali ya kijiografia, nishati, jamii kubwa ya watu, viwanda, utamaduni na ustaarabu na kusema: Ugaidi, vita, umwagaji damu, uingiliaji wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi nyingine na kutokuwepo mazingira mazuri ya ustawi ni miongoni matatizo ya sasa ya Ulimwengu wa Kiislamu. 

Rouhani amesema kuwa, Iran na Malaysia zina misimamo inayofanana kuhusiana na masuala mengi ya kikanda na Ulimwengu wa Kiislamu na zina mtazamo mmoja kuhusiana na udharura wa kuwepo mazungumzo kwa ajili ya kuyapatia ufumbuzi masuala ya Waislamu. 

Vilevile ameashiria uhusiano wa Iran na Japan katika masuala ya kisiasa, kiuchumi na masuala ya mazingira na akasema: Vikwazo vya kidhalimu na vilivyo kinyume na sheria vya Marekani dhidi ya Iran havitadumu na hapana shaka kuwa, nchi nyingi duniani zinataka kuwa na uhusiano mwema na Jamhuri ya Kiislamu. 

3864649

captcha