IQNA

16:20 - January 16, 2020
News ID: 3472377
TEHRAN (IQNA) – Serikali mpya ya mseto nchini Austria imekosolewa kutokana na kufuata sera dhidi ya Waislamu na raia wa kigeni.

Sera mpya iliyotangaa Januari Mosi na serikali ya mseto, ya chama cha mrengo wa kulia kinachojulikana kama Chama cha Watu wa Austria (OVP) na Chama cha Kijani, inaonekana kufuata sera za kibaguzi zilizokuwa zikifuatwa na serikali iliyotangulia.

Mwezi Mei mwaka jana, uchaguzi wa mapema uliitishwa Austria baada ya tuhuma za ufisadi dhidi ya chama cha mrengo wa kulia cha Uhuri wa Austria (FPO) na kiongozi wake wa zamani Heinz Christian Strache. Waustria, hasa raia wa kigeni waishio nchini humo walikaribisha kuunda serikali hiyo ya mrengo wa kulia.

Chama cha Kijani kwa kawaida hupigia debe sera za utunzwaji mazingira, sera za kibinadamu kuhusu uhamiaji na ukimbizi na huwa ni misimamo ya wastani kuhusu kulindwa haki za kidini za waliowachache. Nukta hizo zilipelekea wengi kudhani kuwa muungano mpya unaotawala Austria utaweka mbali sera za chuki dhidi ya Uislamu na wageni.  Lakini kinyume na ilivyotarajiwa, serikali mpya chini ya uongozi wa kiongozi wa OVP Kansela Sebastian Kurz na Chama cha Kijani inatekeleza sera za chuki dhidi ya Uislamu hasa marufuku ya vazi la Hijabu na kupambana na kile kinachotakwa kuwa ni 'Uislamu wa kisiasa. Aidha serikali hiyo mpya ya Austira inawakamata raia wa kigeni na wakimbizi kiholela kwa kushikiwa tu kuwa ni wahalifu na wanaokamatwa hushikiliwa kizuizini bila amri ya mahakama katika utaratibua ambao unajulikana kama 'kifungo cha usalama.'

Mamlaka ya Kiislamu Austraia (IGGO) ambayo inawakilisha Waislamu takribani 800,000 nchini Austria imeilaumu serikali mpya wa kuwa na sera zinazohasimiana na Waislamu. Aidha IGGO imesema imekatishwa moyo na Chama cha Kijani ambacho kinaonekana kuunga mkono sera hizo mpya zilizo dhidi ya Uislamu.

3871618

Tags: iqna ، austria ، waislamu
Name:
Email:
* Comment:
* captcha: