IQNA

19:21 - May 13, 2018
News ID: 3471511
TEHRAN (IQNA) – Idadi ya Waislamu barani Ulaya inatazamiwa kupanda na kufika asilimia 8 na asilimia 2.1 nchini Marekani ifikapo mwaka 2030, imesema ripoti ya Global Muslim Diaspora.

Ripoti hiyo ilitangazwa Jumapili katika warsha iliyofanyika mjini Istanbul, Uturuki kuhusu "Waislamu Katika Nchi Zisizo za Kiislamu Dunaini" .

Warsha hiyo ya siku mbili iliandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uturuki, Idara ya Waturuki Waishio Nchi za Kigeni kwa ushirikiano na Kituo cha Takwimu za Kiuchumi na Utafiti wa Kijamii  (SESRIC) kinachosimamiwa na Jumuiya ya Ushirkiano wa Nchi za Kiislamu OIC.

Ripoti hiyo imesema Austria ndio nchi yenye asilimia kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya na kuongeza kuwa hivi sasa kuna Waislamu milioni 44 wanaoishi barani Ulaya huku kukiwa na Waislamu milioni 5 nchini Marekani.

Kumekuwepo na takwimu zinazokinzana kuhusu idadi ya Waislamu barani Ulaya huku kukiwa njama za kuonyesha idadi ya Waislamu barani humo ni ndogo. Pamoja na hayo, utabiri unaonyesha kuwa idadi ya Waislamu Ulaya itaongezeka maradufu ifikapo mwaka 2050.

Mbali na kuongezeko idadi ya Waislamu Ulaya kutokana na wimbi la wahajiri hivi sasa pia kunashuhudiwa idadi kubwa ya wenyeji asili wa Ulaya wakisilimu na kufuatia Uislamu maishani.

3465812

Name:
Email:
* Comment: