IQNA

Shirika la ndege Marekani latozwa faini kwa kuwatimua wasafiri Waislamu

11:15 - January 26, 2020
Habari ID: 3472407
TEHRAN (IQNA) – Shirika la Ndege la Delta Airlines la Marekani limetozwa faini ya dola 50,000 kwa kuwatimua wasafiri watatu Waislamu ambao tayari walikuwa wameshapanda ndege hata baada ya maafisa wa usalama kusema hakukuwa na tatizo lolote la usalama.

Shirika la Delta limekanusha madai kuwa liliwabagua wasafiri hao katika matukio mawili tafauti lakini limekiri kuwa kulitokea makosa katika kuamiliana na wasafiri hao Waislamu.

Idara ya Usafiri Marekani imelitoza faini shirika la ndege kwa msingi kuwa kuwatimua wasafiri Waislamu kulikiuka sheria za usafiri.  Katika tukio moja la Julai 26 2016 mjini Paris, msafiri alimfahamisha mhudumu wa ndege kuwa alikuwa na waswasi kuhusu wasafiri wawili, mume na mke. Alidai kuwa alikuwa na wasiwasi kutokana na kuwa mwanamke alikuwa amevaa Hijabu na mume wake aliingiza kitu kisichojulikana ndani ya simu yake ya mkononi. Mhudumu wa ndege alidai kuwa alimuona msafiri mwanaume akiandika neno 'Allah' mara kadhaa kwenye simu yake.

Katika tukio jingine la Julai 31, msafiri Muislamu alipanda ndege mjini Amsterdam kwa lengo la kuelekea New York ambapo wasafiri wengine walidai waliona akipewa kifurushi na huo ukawa msingi wa kumzuia kusafiri.

Ubaguzi wa Waislamu wanaosafiri ni jambo la kawaida sasa nchini Marekani hasa tokea Donald Trump aingie madarakani nchini humo.

3873961

captcha