IQNA

11:48 - January 14, 2020
News ID: 3472370
TEHRAN (IQNA) - Baraza la Mahusiano ya Kiislamu Marekani (CAIR) limekosoa ujumbe wa Twitter wa Rais Donald Trump wa nchi hiyo wenye kukejeli Uislamu na Waislamu na kusema ujumbe huo unaweza kuhatarisha maisha ya Wamarekani Waislamu na Masingasinga.

Jumatatu asubuhi alisambza picha zilizohaririwa kwa kutumia photoshop ambazo zinamuonyesha Spika wa Baraza la Wawakilishi katika Bunge la Kongresi ya Marekani Nancy Pelosi na Kiongozi wa Waliowachache Katika Seneti Chuck Shummer, ambapo Pelosi amevishwa Hijabu ya Kiislamu naye Schume akiwa amevishwa kilemba.
CAIR imesema picha hizo zitazidisha zitazidhisha chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na Masingasinga ambao hulengwa kwa kudhaniwa kuwa ni Waislamu kwa sababu wao huvaa vilemba na kufuga ndevu.
Taarifa ya CAIR imesema rais Trump mara kwa mara husambaza fikra zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu na huwateua watu wenye chuki dhidi ya Uislamu mbali na kutekeleza sera zenye kuwabagua Waislamu mfano ukiwa ni ile sera ya kuwapiga marufuku raia wa nchi kadhaa za Waislamu.
Trump alisembaza picha feki ya viongozi hao wa chama cha Democrat wakiwa nyuma ya bendera ya Iran akitaka kuashiria kuwa wanaunga mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Viongozi hao wa ngazi za juu wa chama cha upinzani cha Democrat wamekosoa vikali hatua ya Trump ya kutekeleza kitendo cha kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC katika oparesheni iliyotekelzwa Januari 3 mjini Baghdad nchini Iraq na kulaaniwa kimataifa.
Wiki iliyopita, Pelosi alieleza kupitia taarifa kwamba, kufuatia mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani, yaliyofanywa kwa amri ya Trump; na kutokana na kuongezeka hali ya wasiwasi na mivutano katika eneo la Asia Magharibi, baraza hilo litapigia kura mpango ambao endapo utapitishwa, utapunguza mamlaka ya Trump ya kuitumbukiza Marekani kwenye mizozo ya kijeshi.
Katika taarifa yake hiyo, Pelosi alibainisha kuwa: "Ijumaa iliyopita, serikali ya Trump iliwashambulia maafisa waandamizi wa kijeshi wa Iran katika shambulio la kijeshi la kichochezi na lisilo na mlingano."
Bi Pelosi alisisitiza katika taarifa yake hiyo kwamba, hatua hiyo ya Ikulu ya White House ilichukuliwa bila kushauriana na bunge la nchi hiyo la Kongresi na imepelekea kushadidi mivutano na Iran katika eneo la Asia Magharibi.

3871448

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: