Alaa na Gamal Mubarak pamoja na wengine saba walikuwa wanakabiliwa na mshtaka ya kupata faida kinyume cha sheria katika mchakato wa kuiuza Benki la Al Watani ya Misri ambayo ilinunuliwa na Benki ya Kitaifa ya Kuwait mwaka 2007.
Wawili hao walisisitiza hawana hatia na walihuhduria kikao cha hukumu hiyo katika Mahakama ya Jinai ya Cairo. Wawili hao walitiwa mbaroni baada ya mwamko wa mwaka 2011 na walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela mwaka 2015, wakiwa pamoja na baba yao.
Ndugu hao wawili waliachiliwa huru punde baada ya hukumu hiyo kwa sababu tayari walikuwa wameshakaa muda mrefu kizuizini huku baba yao naye akiachiliwa huru mwaka 2017 baada kufutiwa mashtaka wa kuamuru waandamanaji wauawe.