Mkuu wa Taasisi ya Mashindano ya Qur'ani ya Iran Karim Dolati amesema mashindano hayo yalikuwa yamepangwa kufanyika Aprili 10-14 yataakhirishwa ili kuzuia kuenea ugonjwa wa Corona ambao umesababisha hofu duiani kote.
Ameongeza kuwa, yamkini mashindano hayo yakafanyika baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani yaani kuanzia Mei 24. Amesema maelezo zaidi yatatolewa katika siku zijazo.
Maambukizi ya kirusi cha corona yalianzia katika mji wa Wuhan nchini China Desemba mwaka uliopita wa 2019 na inavyoonesha chanzo chake ni wanyama wasio wa kufuga.
Mbali na mikoa 30 ya China, hivi sasa kirusi hicho kimesambaa kwenye nchi zaidi ya 40 duniani huku watu zaidi ya 81,000 wakiwa wameambukizwa ambapo 78,000 wako nchini China. Aidha n kirusi cha Corona kimeua watu wasiopungua 2,800 ambapo miongoni mwao 2,717 wako nchini China.