IQNA

14:27 - March 04, 2020
News ID: 3472530
Katika siku za hivi karibuni, watu 43 wasio na hatia, aghalabu wakiwa ni Waislamu, wameuawa nchini India katika hujuma za Wahindu wenye misimamo mikali na ya kufurutu adha.

Aidha magaidi hao wa Kihindu wameteketeza moto misikiti, makumi ya nyumba na madika ya Waislamu. Aghalabu ya waliopoteza maisha wameuawa kinyama kwa kupigwa kwa fimbo au kupigwa mawe huku polisi wakiwa ni watazamaji wa jinai hizo.

Kufuatia maandamano ya hivi karibuni ya kulalamikia sheria yenye utata ya uraia nchini India ambayo inawabagua Waislamu, sasa Wahindu wenye misimamo ya kufurutu ada wamekithirisha hujuma zao dhidi ya Waislamu.

Hujuma hizo za Wahindu dhidi ya Waislamu zinafanyika kwa msingi wa ile itikaadi ya Hindutva ambayo ni ya utaifa wenye kufurutu ada wa wafuasi wa dini ya Kihindu ambao wanaamini kuwa India ni milki yao na raia wengine wote nchini humo ni wa daraja la pili.

Wiki moja baada ya wanagambo wa Kihindu kuwahujumu Waislamu, miili ya Waislamu ingali inaendelea kupatikana.

Serikali ya India imekiri kuwa Wahindu wenye misimamo ya kufurutu adha wametekteza moyo nyumba 122, maduka 322 na magari 301 ya Waislamu.

Vyombo vya mahakama India vimesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu jinai dhidi ya Waislamu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya ya uraia India, ni ruhusa kupatiwa uraia wahajiri wa jamii za Wahindu, Mabudha na hata Wakristo wanaotokea katika nchi jirani za Pakistan, Bangladesh na Afghanistan, huku ikizuia kupewa uraia Waislamu wanaotoka katika nchi hizo.

3882992

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: