IQNA

12:34 - March 25, 2020
News ID: 3472600
TEHRAN (IQNA) – Serikali ya Kuwait imetangaza mpango wa kuanzisha masoo ya kuhifadhi Qur'ani kupitia intaneti baada ya madrassah za Qur'ani nchini humo kufungwa kwa muda ili kuzuia kuenea ugonjwa wa COVID-19 maarufu kama kirusi cha corona.

Wizara ya Wakfu ya Kuwaita imesema itaandaa masomo hayo ya Qur'ani kupitia intaneti.

Naibu Waziri wa Wakfu nchini Kuwait anayesimamia masuala ya Qur'ani na masomo ya Kiislamu Fahd al Jinfawi amesema mpango huo umeratbiwa baada ya amri ya serikali ya kufunga madrassah na vyuo vyote vya kieleimu nchini humo ili kuzuia kuenea corona.  Aidha ametoa wito kwa wanafunzi kujisajili kupitia tovuti ya wizara ili kuweza kushiriki katika masomo hayo ya kuhifadhi Qur'ani.

Misikiti pia imefungwa kote Kuwait kwa zaidi ya siku 10 sasa.

Hadi kufikia Jumanne watu 191 walikuwa wameambukizwa corona nchini Kuwait.

Kwa mujibu wa takwimu za karibuni kabisa, zaidi ya watu 423,000 wameambukizwa covid-19, zaidi ya 109,000 miongoni mwao wamepata nafuu na wengine wasiopungua 18,000 wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya kirusi hicho.

3887028

Name:
Email:
* Comment:
* captcha: