IQNA

Qarii maarufu wa Saudia aambukizwa corona akiwa London

11:38 - April 01, 2020
Habari ID: 3472622
TEHRAN (IQNA) – Qarii (msomaji) maarufu wa Qur’ani Tukufu kutoka Saudi Arabia, Abubakr al-Shateri ameambukizwa ugonjwa wa COVID-19 au corona.

Kwa mujibu wa taarifa, Sheikh al-Shateri aliambukizwa ugonjwa huo alipokuwa safarini London, Uingereza.

Sheikh Abdu Aziz al-Nafis, Imamu wa Msikiti wa Jamia wa Mji wa Kuwait, ambaye aliandamana na al-Shateri mjini London, amethibitisha habari hiyo. Al-Nafis ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa, yeye na al-Shateri walikuwa walikaa katika nyumba moja London kabla ya kurejea makwao. Amemuomba Mwenyezi Mungu SWT ampe shifaa qarii huyo wa Qur’ani kutoka Saudia.

Al-Shateri alizaliwa mwaka 1980 mjini Jeddah na hivi sasa ni miongoni mwa wasomaji maarufu wa Qur’ani nchini Saudia. Aidha yeye ni Imamu wa Msikiti wa al-Furqan mjini Jeddah.

Hadi hivi sasa kuna kesi 1,563 za wagonjwa wa  corona nchini Saudia huku wengine 10 wakiripotiwa kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo. Saudia Arabia imefunga misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina ili kuzuia kuenea corona nchini humo.

3888187

captcha